| Baadhi ya wafanyabiashara Nchini wakimsikiliza kwa makini Mjenga Uwezo wa
Kimataifa wa Masuala ya Kibiashara kutoka Singapore,Harish Babla wakati wa warsha ya mazungumzo ya kuwapatia mafunzo
ya uwezo wa kufanya biashara Kimataifa na Kitaifa kwa ufasaha kwa wafanyabiashara
hapa nchini,Warsha hiyo iliandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya Shrijee’s
Traders jana jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam, April 2, 2016, Shrijees Traders wamiliki na
waendeshaji wa supermarket za Shrijees hapa nchini jana waliandaa mazungumzo ya
kibiashara yaliyoongozwa na mjenga uwezo wa kimataifa kutoka nchini Singapore,Harish Babla yalibeba
ujumbe “Kuibuka kwa viongozi wapya
katika biashara ni kichocheo katika dunia yenye mkanganyiko”
Harish Babla, aliwaongoza washiriki wa mazungumzo hayo ya kutiana
moyo ambao ni wafanyabiashara juu ya sifa saba ambazo lazima kiongozi awe nazo ili kuweza kuendelea kuwepo katika
dunia yenye mvurugano wa aina mbali mbali.
Mazungumzo hayo yaliongezewa uhai na stadi iliyofanywa Chuo kikuu cha
Oxford cha Uingereza chini ya Dkt Johari.
Babla alisema, “Dunia imekuwa kama kijiji na hakuna kiongozi katika
biashara anaweza kudharau ulimwengu wan je. Zaidi mno, viongozi katika biashara
lazima wafikirie mbali zaidi, wawe wenye uthubutu, wabunifu, wenye uelewa wa
kutosha juu ya teknalojia na dunia”. Aliongeza Ni muhimu kwa viongozi wa kibiashara katika nchi
zinazoendelea kuchukua muda wao wa ziada nje ya kazi kujifunza juu ya mambo
mbali mbali,”
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shreeji Traders ambao ndiyo waandaaji na
wadhamini wa tukio hilo Vasant Champsi alisema “Wakati makampuni hapa Tanzania
yakiendelea kushirikiana na dunia ya nje, ni muhimu kuwa makini kusikiliza
mawazo mapya pamoja na sauti zenye uzoefu tofauti ambazo zitasaidia biashara
zetu kufanya vizuri ndani ya nchi n ahata nje ya nchi,
Mkurugenzi huyo aliongeza “Shrijees Traders tumeamua kuandaa tukio
hili la aina yake hapa Tanzania kwa
kumleta mtu mwenye uzoefu na kiongozi mwenye mawazo ya kibiashara ambaye
amezaliwa Tanzania na leo amekuja kutushikisha uzoefu na mawazo yake katika
masuala ya kibiashara. Tunaamini wafanyabiashara waliohudhuria warsha hii
wamenufaika na mafunzo haya na ninapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara na makampuni mengine kuiga mfano na kuwaleta
wazungumzaji wengine kwa maendeleo ya nchi yetu,”
Frank
Goyayi mmoja ya wafanya biashara wakubwa hapa nchini na mshiriki wa warsha hiyo
alisema, “Harish, kupitia njia hii ya kubadilishana mawazo kwa mazungumzo yenye
hadithi na mifano, ndani ya dakika 90 tumesafiri duniani kote na kuona umuhimu
wa viongozi wapya katika biashara,”
Harish
Babla, ni mzaliwa wa Tanzania ambaye ana
uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika masuala ya kibiashara na ameshiriki kujengea
uwezo makampuni na wafanyabishara wengi duniuani kupitia matukio ya kujifunza.
|
No comments:
Post a Comment