JESHI
la Kujenga Taifa (JKT), limetoa siku saba kwa wabunge wa majimbo 18
yaliyopo ndani ya mikoa saba nchini kuhakikisha wanachukua madawati yao
yaliyotengenezwa na jeshi hilo kabla ya Agosti 30, mwaka huu.
Madawati
hayo 9,666 ni kati ya 30,000 ya awamu ya kwanza yaliyotengenezwa na
jeshi hilo baada ya Ofisi ya Bunge kulipa zabuni ya kutengeneza madawati
60,000 kwa Sh bilioni tatu.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ),
Dk Hussein Mwinyi, alisema jeshi hilo limelikabidhi Bunge madawati
30,000, lakini madawati 9,666 kati ya hayo hayajachuliwa.
Hata
hivyo, alisema kulingana na mgawo ambao jeshi hilo lilikabidhiwa na
Kamati ya Bunge, madawati hayo yaligawanywa katika majimbo ya mikoa
tisa, lakini hadi sasa majimbo 18 katika mikoa saba hayajachukua
madawati hayo.
Aliitaja
mikoa iliyopo kwenye mgawo huo na idadi ya madawati kwenye mabano kuwa
ni Tanga ( 6,444), Njombe (3,222), Iringa (3,790), Mbeya (3,759), Mbeya
Songwe (3,222), Rukwa (1,611), Ruvuma (4,833), Unguja (3,200) na Pemba
(1,800).
“Mpaka
sasa madawati yaliyokwishachukuliwa ni 22,721, madawati 9,666 kati ya
30,000 yaliyokwishakamilika sawa na asilimia 30 hayajachukuliwa na
majimbo husika. Tunawaomba wabunge husika waje kuyachukua kabla ya
Agosti 30, vinginevyo tutaziomba mamlaka husika ziyagawe kwenye maeneo
yenye mahitaji,” alisema.
Dk
Mwinyi aliyataja majimbo na mikoa ambayo hadi sasa hayajachukua
madawati hayo kuwa ni Tanga katika majimbo ya Kilindi na Pangani (1,611)
na Njombe majimbo ya Makambako, Ludewa, Wanging’ombe na Makete (2,148).
Maeneo
mengine ni Iringa katika majimbo ya Iringa Mjini, Mbeya Mjini na Mbeya
Vijijini (91,611), Ruvuma Jimbo la Tunduru Kaskazini ( 537) na Mbeya
katika majimbo ya Ileje, Kyela, Rungwe na Busokelo ( 2,148).
Mengine
ni Songwe ( 537) na Kwela, Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini (Rukwa)
(1,611). Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, kutochukuliwa kwa madawati hayo
kunasababisha kukosekana kwa nafasi ya kuweka madawati mengine
yanayotengenezwa kwenye vituo mbalimbali vya JKT.
Pia,
alisema yanapoendelea kubaki mahali hapo yanapigwa jua, kunyeshwa na
kupungua ubora. Pamoja na hayo, alisema kuwa awamu ya pili ya madawati
30,000 inaendelea vyema kwa kuwa tayari madawati 20,000 yamekamilika na
yanaweza kuchukuliwa na kugawanywa panapohusika.
Alisema, “madawati 10,000 yaliyobaki yatakamilika kabla ya Oktoba 30,000 kama ilivyopangwa na yatagawanywa katika majimbo 51”.
No comments:
Post a Comment