Kijana
Petro Magoti kutoka Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, aliyeko
Ujerumani kwa masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa, akiagana na
mmoja wa wamiliki wa viwanda vikubwa Duniani, Prof. Karl Knoop, baada ya
kuzungumza naye, mjini Berlin, Ujerumani, juzi. Kushoto ni Meya wa
mji wa Bugermeister,
David Osthotlhoff.
NA BASHIR NKOROMO
Katika
kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha Tanzania
katika mapinduzi ya viwanda vikubwa na Vidogo, Kijana Petro Magoti
ambaye ni mwakilishi pekee kwa Tanzania aliyeko nchini Ujerumani, kwenye
mafunzo ya uongozi na uhusiano wa kimataifa, amekutana na mmoja wa
wamiliki wa viwanda vikubwa Duniani, Prof. Karl Heinz Knoop na kufanya
mazungumzo naye ili kumshawishi kuja kuwekeza nchini.
Akizungumza
kutoka nchini Ujerumani, Magoti amesema leo kwamba, Prof. Knoop ambaye
anamiliki viwanda katika nchi 17 Barani Ulaya na katika nchi nne katika
bara la Afrika, katika mazungumzo yao, Prof. Knoop ameonyesha dhamira ya
kuwekeza Tanzania katika meneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na Kilindi
mkoani Tanga.Magoti amesema, Prof, Knoop, amefikia dhamira hiyo baada ya kumweleza kwa kina fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania, na namna nchi ilivyojipanga kuwapokea kwa ukarimu wawekezaji kutoka nchi za nje ikiwemo Ujerumani, lengo likiwa kuifikisha nchi kuwa yenye viwanda na hivyo kuwezesha wananchi wengi wakiwemo vijana kupata ajira za uhakika.
“Katika mazungumzo yetu, Prof. Karl Heinz Knoop ameeleza kuwa na dhamira ya kuwekeza Tanzania ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuondoa umasikini, hata hivyo akasema, awali amewahi kuonyesha azma hiyo kwa wakati, lakini akakumbana na changamoto lukuki ikiwemo kupewa eneo la kujenga viwanda vikubwa vya mashine za kilimo kama vile Matrektar, Mashine za kupanda mbegu, Kuvuna na kukausha mazao, na Maghala makubwa ya kuhifadhia vyakula na kiwanda cha magari makubwa ya mizigo”, aalisema Petro.
No comments:
Post a Comment