
Mchezaji wa timu ya Ndanda FC ya
Mtwara akikokota mpira huku mchezaji wa Simba Laudit Mavugo akimfukuzia
katika mchezo wa Ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam jioni hii . Timu zote zimepata magoli katika
kipindi cha kwanza Simba ikijipatia goli lake kupitia kwa Laudit
Mavugo huku Ndanda FC ikisawazisha kupitia mchezaji Omary Mponda.
Katika kipindi cha pili wachezaji
wa timu ya Simba Fredrick Blagnon na Shiza Kichuya wamefanikiwa
kuifungia timu yao magoli mawili na kuifanya Simba kushinda mchezo huo
3-1 dhidi ya Ndanda FC.

Mchezaji wa Fredrick Magnon
akiruka juu na golikipa wa timu ya Ndanda FC Jackson Chove huku
wachezaji wa timu hiyo wakiangalia wakati mchezo huo wa ligi kuu
unaendelea.

Wachezaji wa Ndanda FC na SimNdanda ba wakiwania mpira golini mwa lango la FC.

Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa nguvu mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Ndanda FC.

Mashabiki wa timu ya Ndanda FC
wakiishangili timu yao wakati ikimenyana na timu ya Simba ya Dar es
salaam kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.

Mashabiki wa timu ya Simba wakionyesha kumlaumu mwamuzi hayupo pichani kutokana na baadhi ya maamuzi katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment