Mkuu
wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe, amekutana na wanahabari
kuelezea tukio la juu ya taarifa zilizozangaa mjini Singida, kwamba
Rahel Erasto (28) aliyefariki muda mfupi baada ya kujifungua kwa njia ya
upasuaji, kafufuka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa.
Mhandisi
Mtigumwe alisema kuanzia mapema asubuhi mwili huo ulikuwa ukifanyiwa
uchunguzi wa kina na kundi la wataalam wa afya likiongozwa na Daktari
bingwa kutoka Makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Dk. Ahmed Mataka.
 |
| Kaimu
mganga mkuu mkoa wa Singida,Dk.Ramadhan Kabala,akitoa taarifa juu ya
maiti kufufuka ikiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya
mkoa mjini hapa. |
 |
| Kaimu
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,SSP Mayala Towo,akitoa
taarifa juu ya kushikiliwa kwa mwajiriwa wa hospitali ya mkoa mgambo
Emmanuel Daghau (28) kwa tuhuma ya kutoa taarifa za uongo kwa ndugu wa
marehemu Rahel na jeshi la polisi juu ya kufufuka kwa maiti akiwa chumba
cha kuhifadhia maiti. |
 |
| Baadhi
ya waombolezaji wa msiba wa Rahel Erasto aliyefariki dunia na kudaiwa
kufufuka.Rahel alifariki dunia muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji
kwa ajili ya mtoto kutolewa tumboni. |
 |
| Mkuu
wa mkoa wa Singida,mhandisi Mathew Mtigumwe,akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya taarifa zilizozangaa mjini
Singida,kwamba Rahel Erasto (28) aliyefariki muda mfupi baada ya
kujifungua kwa njia ya upasuaji,kafufuka akiwa chumba cha kuhifadhia
maiti hospitali ya mkoa.
(Picha zote na Nathaniel Limu).
|
No comments:
Post a Comment