Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameziagiza
halmashauri zote nchini zilizopata fedha kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu ya madarasa na vyoo katika shule za msingi zitumike kwa
wakati badala ya kuchelewesha ujenzi huo kwa visingizio visivyo na
msingi na hivyo kupelekea wanafunzi kuendelea kusoma katika mazingira
magumu.
Prof.Ndalichako
ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule za msingi,sekondari na vyuo
katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri na kubaini kuwapo
kwa uzubaifu usiokuwa na sababu katika kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo
ikiwemo shule ya msingi Mbawala ambayo imepokea shilingi milioni
miamoja na 91.8 lakini imeshindwa kuanza ujenzi wakati imepokea fedha
hizo tangu mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumzia
kuchelewa kuanza kwa ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara
Omar Kipanga amesema sababu kubwa ya uchelewaji imetokana na
ugumu wa kubomoa jengo chakavu
Mradi
huo wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa,vyoo na ukarabati wa majengo
unafanyika katika baadhi ya halmashauri nchini umegharimu shilingi
bilioni 14,wakati mkoa wa Mtwara umelenga katika shule tano na mpaka
kukamilika kwake utagharimu shilingi milioni 868.


No comments:
Post a Comment