![]() |
| Waziri Ummy akiongea na watoto waishio kwenye kituo cha watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Uyacho |
![]() |
| Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akisalimiana na mtoto ambaye nyumba yao ilianguka kwa tetemeko na sasa wanaishi kwenye Tenti |
![]() |
| Waziri Ummy akiongea na walezi wa kituo cha kulelea watoto cha Uyacho huku akimbeba mtoto Bahati aliyeokotwa na msamaria mwema mkoani Kagera,Kituo hicho ni kati ya nyumba zilizoanguka baada ya tetemeko na hivyo kuhamishia shughuli zao kwenye Tenti(Picha na Catherine Sungura-WAMJW) |
![]() |
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
amekataza kulipisha pesa za vipimo kwa wagonjwa wote wenye kadi za Bima
ya Afya.
Waziri
Mh.Ummy Mwalumu ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi walioenda
kupata matibabu kwenye kituo cha afya cha Rwamishenye.
“Ni
marufuku kuwalipisha wagonjwa wale wote wenye bima ya mfuko wa afya ya
jamii ama tele kwa tele au kadi za bima ya afya labla kama dawa hakuna
ndio wanaweza kununua”alisema
Aidha,
amewataka wananchi kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe hasa wale ambao
hawajakata tele kwa tele hasa vijijini ili waweze kupata huduma za afya
bila kulipa kila waendapo kupata huduma
“Mnajua
hakuna anayejua leo ama kesho ataugua, na magonjwa hayapigi hodi na
wakati mwingine yanakukuta hauna akiba ya fedha,ila ukiwa na bima wakati
wowote unapata matibabu”
Hatahivyo
amewakumbusha watoa huduma za afya kuweza kutoa huduma kwa kufuata
kanuni na weledi wao ili kuweza kuondoa malalamiko mengi toka kwa
wananchi.
“Mgonjwa
anapofika kituo cha afya anakuwa aidha amechanganyikiwa au ana mawazo
mengi hivyo anahitaji kauli nzuri,faraja na huduma zinazostahili,hivyo
wakuu mganga mkuu wa kituo unatakiwa kukemea na kukumbusha maadili na
viapo vya maadili vya watoa huduma”
Aliwasisitizia
kuwa bima ya afya ya jamii inawahudumia wanachama sita kwenye familia
hivyo itawasaidia hasa pale mtoto anapotimiza umri wa miaka mitano hivyo
atahitaji kulipia huduma zote za afya.
Kwa
upande wa uzazi wa mpango Waziri Ummy aliwataka akinamama hao wazae kwa
kufuata uzazi wa mpango kwani maisha ya siku hizi ni magumu
“Hatusemi
kwamba mzae watoto wachache lakini mzae kwa mpangilio,’Mhe.Rais
amewezesha elimu bure” ila mtoto anahitaji malezi,maziwa pamoja na
malazi.
|






No comments:
Post a Comment