![]() |
| Rais Obama amesema Donald Trump hafai kuwa rais Marekani
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa
wito kwa viongozi wakuu wa chama cha Republican kuondoa rasmi uungaji
mkono wao kwa mgombea wa chama hicho Donald Trump.
Akiongea katika
mkutano wa kampeni wa kumuunga mkono mgombea wa chama cha Democratic
Hillary Clinton, Bw Obama amesema haina maana kukemea matamshi ya
kudhalilisha ya Bw Trump kuwahusu wanawake bila kujitenga na mgombea
huyo.Akihutubu Greensboro, North Carolina, Jumanne jioni, Rais Obama alishangaa ni vipi wanasiasa wa Republican bado wanataka Bw Trump awe rais. "Hali kwamba sasa kuna watu wanaosema: 'Sikubaliani kamwe na hili, napinga hilo kabisa ... lakini bado tunamuidhinisha.' Bado wanafikiri anafaa kuwa rais, hilo kwangu halileti maana," alisema. Bw Obama alisema matamshi ya Bw Trump kuhusu wanawake hata yanaweza kumfanya akose hata kazi ya dukani. "Sasa unapata hali ambapo huyu bwana anasema mambo ambayo hakuna anayeweza kuyavumilia hata kama mtu huyo angekuwa akiomba kazi (maduka ya) 7-Eleven," alisema. BBC Bw Obama alikatizwa mara kadha akitoa hotuba na wapinzani wa Bi Clinton lakini alionekana kutoathirika. Badala yake aliwajibu: "Hii ni demokrasia. Hili ni jambo zuri sana."Watu hao waliokuwa wakimzomea walitolewa nje na maafisa wa usalama |
October 12, 2016
JITENGENI NA TRUMP-OBAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment