
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo
(kushoto) akifugua kongamano la nne linalohusu gesi na mafuta
lililoambatana na maonesho , lililokutanisha wadau mbalimbali kutoka
makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo
vikuu, wizara na taasisi za serikali jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo
(kushoto), akibadilishana mawazo na Kaimu Kamishna wa Nishati na
Maendeleo ya Petroli, James Andilile (kulia) katika kongamano hilo

Kutoka kulia; mwakilishi kutoka
Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu, Kaimu
Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk.
Juliana Pallangyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zinawasilishwa katika kongamano hilo.

Washiriki kutoka makampuni
yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu,
wizara na taasisi za serikali wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa
na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kongamano hilo.


No comments:
Post a Comment