Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MADEREVA wa matipa ya mchanga
,wanaotumia barabara kuu ya Dar es salaam –Morogoro, wamefanya mgomo
baridi ,kulalamikia wakala wa barabara (TANROADS)mkoani
Pwani,unaowakamata kutokana na kutofunga mchanga vizuri na kuwapiga
faini ya sh.500,000.
Madereva hao waliweka mgomo huo
katika eneo la Tamco ambapo ndipo watendaji wa wakala huo walikuwa
wakiwasimamisha kwa ajili ya kukagua wale waliojaza mchanga hali
inayosababisha kuchafua miundombinu ya barabara.
Dereva Martine Magari na Emmanuel
Shao,walisema ni kweli wapo madereva wasiofunga vizuri maturubai ya
magari yao lakini tatizo kubwa ni kukosa elimu ya kufunga kwa ubora .
Shao aliziomba idara ama mamlaka
husika kutoa elimu juu ya sheria mbalimbali kwani inakuwa sio rahisi
kuelewa sheria zote zinazotungwa bila kupatiwa elimu ya kutosha.
“Unaona fuso dogo kama lile,huwezi
amini ni sh.500,000 kikweli ni kubwa ,sasa unakuta tunalalamika
kutokana na kwamba hatujui lolote kuhusu sheria zao”
“Halafu hatujafundishwa kufunga
hooks wanavyotaka wao wakala wa barabara,kila mtu anaufungaji wake
lakini endapo watatuelewesha vizuri haina shida .
“Sasa wao wanapanda juu ya gari na kuchokonoa chokono matokeo yake ndio inakuwa shida ,mchanga unamwagika”alisema Shao.
Magari aliutaka wakala huo kukagua
kwa macho na sio kupekenyua maturubai kwa kuingiza mikono kwani kwa
kufanya hivyo ni lazima mchanga mwagike .


No comments:
Post a Comment