Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba,
(kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service,
Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme
(transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya
TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia
mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa
KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika
la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za
Kimarekani
309.26
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said.
SHIRIKA
la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na makampuni
matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), wa Msongo wa
Kilovolti 400 utakaounganisha Tanzania na Kenya.
Hafla
ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao
makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika hilo la Umeme
linalomilikiwa na serikali, limetiliana saini mikataba hiyo na makampuni
ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.
Akizungumz
wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi,
Felchesmi Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita
414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa
Tanzania na Kenya.
Kisha
Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa
kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la
mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya
umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.
“
Napana niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa
inayotekelezwa na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati
2000 katika pande zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mramba.
Akifafanua
zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa
na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya
Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni
309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.
“Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa onyo kwa wakandarasi waliopewa
kazi hiyo kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
“
Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama
ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa
mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO
hatutakubaliana na hilo.” Alionya Mhandisi Mramba.
Naye
mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki
hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo
lote la Afrika.
Kwa
upande wake, MAfisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, naye
aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya
Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama
huu uliosainiwa leo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues
Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba
Mhandisi
Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera
Hadzialjevic, wakisaini mkataba kutekeleza mradi huo
Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati









No comments:
Post a Comment