
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni alipowasili katika Gereza Kuu la Karanga, Mkoani
Kilimanjaro wakati alipotembelea kiwanda cha viatu kilichopo gerezani
haapo ili kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali hasa viatu. Naibu
Waziri huyo amelitaka Jeshi hilo kuzidi kuboresha bidhaa za viatu hivyo
ili kujipatia soko kubwa ndanni ya nchi na kutekeleza agizo la Rais
Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanattumia viatu
vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Karanga,
Kamishna Msaaidizi Mkwiche mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara
katikaa Kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo ili kujionea
uzalishaji wa bidhaa za viatu ambavyo Rais Magufuli alitaka majeshi
yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa viatu
katika kIwanda cha Gereza la Karanga kutoka kwa Fundi Mkuu wa Kiwanda
hicho Ali Jambaraga wakati alipofanya ziara yake kwenda kujionea
uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini pia ametaka wazidi kuzalisha
bidhaa bora zaidi ili kuteka soko la ndani na je ya nchi ikiwa ni pamoja
na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini
kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.


No comments:
Post a Comment