
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masaun akionyeshwa Mpaka katika picha unaotenganisha
Tanzania na Kenya ulioko Holili wilayani Rombo alipofanya zaiara ya siku
moja ya kikazi kuangalia mipaka hiyo na kutoa maelekezo kwa wahusika wa
kulinda mipaka hiyo namna ya kuweza kukabilina na changamoto zilizopo
katika mpaka huo.
,,,,,,,,,,,,,,,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Masauni avitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzidi
kuimarisha ulinzi katika mipaka ili kushirikiana na Serikali katika
mpango wa kupambana na uhalifu nchini.
Masauni aliyasema hayo leo wakati
alipofanya ziara katika mipaka ya Tarakea na Holili iliyopo mkoani
Kilimanjaro ili kujione changamoto zinazojitokeza katika mipaka hiyo
ambapo tarifa zinaonyesha kwamba kuna njia zisizo rasmi zaidi ya 265
zinazotumiwa kuptisha bidhaa za magendo na wahamiaji haramu
Katika ziara hiyo Naibu Waziri
Masauni alivitaka vyombo vyote vya ulinzi na Usalama nchini kuhakikisha
vinaashirikiana kila mtu kwa nafasi yake ili kupambana na uhalifu wa
kupitisha bidhaa za magendo zinazopitishwa katika mipaka hiyo na
kuikosehsa serikali mapato.
Masauni alisema kuwa Serikali ya
awamu ya Tano ina dhamira ya kupeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo
ni lazima kwa vyombo hivyo kudhibiti biashara zote zinazopita kimagendo
mipakani humo lakini pia kuepuka rushwa ili kupiga hatua mbele za
kimaendeleo.
Pamoja na kuwapo kwa changamoto
ya nguvu kazi na vitendea kazi serikali itahakikisha inaaandaa maofisa
wa kutosha mipakani humo ili kuongeza nguvu kazi wakati wa operesheni
zao na doria wakati wote.
Aidha Masauni ametoa rai kwa
watumishi wa vyombo hivyo kujiepusha na tabia ya kushirikiana au
kuwaficha wafanyabiaashara wanao jihusishaa na biashara ya maagendo.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Kilimaanjaro Kamishna Msaidizi Mwqaandanizi Wilbrod Muutafungwa
almueleza naibu Waziri huyo licha ya changamoto zilizopo wanaendelea
kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka kwa kufanya doria mara
kwa mara licha ya kwamba wafanyabiashara hao wa bidhaa za magendo
kutumia mbinu mbalimbali kukwepa ushuru lakini Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro limeweza kuwatia mbaroni.


No comments:
Post a Comment