
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel
Manyele (kulia), akitoa hotuba wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa
wanafunzi na walimu Bora wa masomo ya Kemia na Baiolojia kwa kidato cha
Nne na kidato Tano 2014/2015 iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya
Mkemia Mkuu wa Serikali.

Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Bw. Michael John (kulia) akitoa hotuba kabla ya kukabidhi zawadi
kwa Wanafunzi na Walimu Bora wa masomo ya Kemia kwa Kidato cha Nne
waliomaliza mwaka 2014 na cha Sita 2015. Jumla ya wanafunzi Ishirini na
Nne (24) na walimu wane (4) walifanikiwa kupewa zawadi kwenye hafla
iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali, Jijini
Dar es Salaam.

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya
Serikali, Dkt. Jim Yonazi (kulia) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya
wazazi wa wanafunzi waliopata zawadi kwa kufanya vizuri kwenye masomo ya
Kemia na Baiolojia kwa Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Tano 2015. Dkt
Yonazi alimsindikiza kijana wake Yonazi Charles Senkondo kwenye hafla
hiyo


Wanafunzi Bora wa masomo ya Kemia na
Baiolojia kwa Kidato cha Nne na Tano kwa mwaka 2014/2015 wakitambulishwa
wakati wa hafla ya kuwapa zawadi iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi
ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi, Bw. Michael John,
akimkabidhi zawadi mwanafunzi, Yonazi Charles Senkondo (kulia) baada ya
kuwa mwanafunzi bora kwenye masomo mawili ya Kemia na Baiolojia kwa
kidato cha Sita mwaka 2015.


No comments:
Post a Comment