
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Watendaji
wa Mahakama nchini wamehimizwa kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu, ili
kurejesha imani kwa wananchi juu ya chombo hicho muhimu katika utoaji wa
maamuzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alitoa kauli hiyo jana kwenye Mkutano
wa robo mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na
Geita uliofanyika Jijini Mwanza.
Mongella
alisema watendaji wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanapaswa
kutenda haki katika shughuli zao na kuhakikisha mchango wa mahakama
katika utoaji wa haki unaonekana kwa wananchi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Majaji na Mahakimu tawi la Mwanza, Francis Kishenyi,
ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe, alisema miongoni
mwa malengo ya chama hicho ni kuhakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo
Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya mahakama.
Pamoja
na mambo mengine, mkutano huo umejadili masuala mbalimbali ikiwemo
maadili ya viongozi wa Umma katika kuwatumikia wananchi


No comments:
Post a Comment