
Naibu Waziri Ofisiya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kulia akifafanua jambo
kuhusu utunzaji wa mazingira alipokuwa akiongea na uongozi wa Mkoa wa
Tabora (hawapo pichani) leo katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe
Aggrey Mwamri na kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa Dk. Thea M. Mtara.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora
Dk. Thea Mtara akisoma Repoti ya Mazingira ya Mkoa kwa Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina mapema
leo kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa mazingira Mkoani Tabora.

Washiriki wa mkutano wa viongozi
wa Mkoa wa Tabora na waandishi wa habari wakati Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano namazingira Mhe. Luhaga Mpina akipokea maelezo
kuhusu ripoti ya mazingira ya Mkoa wa Tabora.
(Habari na Picha na Evelyn Mkokoi.)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, amewataka viongozi wa Mkoa
wa Tabora kuwachukulia hatua za kisheria waharibifu wa mazingira mkoani
humo, na kushauri Mahakama kuongeza jitihada kwa kuhakikisha mazingira
yanalindwa kwa kusikiliza haraka kesi za uharibifu wa mazingira
zinazopelekwa mahakamani na pia ziende kwa wakati.
Mpina ameyasema hayo Mkoani Tabora
alipokuwa akipokea repoti ya mazingira ya Mkoa iliyosomwa na katibu
tawala wa mkoa Dkt Thea Mtara mapema leo kabla ya kuanza ziara yake ya
ukaguzi wa mazingira mkoani humo.
Aliongeza kuwa suala la usafi wa
mazingira linapaswa kupewa kipaumbele na ifikie mahali kila Halmashauri
na manisapaa itoe ripoti yaukweli kuhusu usafi wa mazingira na upandani
wa miti katika halmashauri zao na watendaji wavivu na wasiojiweza
wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua.
Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa
kusema kuwa hakuna haja ya kuwa na vyombo vya utendaji kama NEMC au
wakala wa taifa wa misitu katika kila kijiji kwani mfumo wa selikali
uliyo unajitosheleza, hivyo kila mtumishi anapaswa kuwajibika kwanafasi
yake.
“nimeskia kumekuwa na uharibifu wa
mazingira hapa Tabora unaofanywa na wachimbaji wadogo pia na
wawekezaji, tuna haja ya kujirithisha kama wawekezaji hawa wanafuata
sheria za nchi kama vile kupata vyeti vya mazingira kupitia Baraza la
Hiafadhi na Usmamizi wa Mazingira (NEMC).” Alisisitiza Mpina.
Awali, akisoma Ripoti ya mazingira
ya Mkoa wa Tabora, katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Thea Mtara, alisema
kuwa mkoa umekuwa uikabiliwa na changamoto mbali mbali za uharibifu wa
mazingira ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa kokoto, uharibifu wa kukoboa
miti kwa ajili yahifadhi ya tumbaku, uchimbaji wa madini na uharibifu
katika hifadhi za taifa kutokana na uvamizi wakulima na wafugaji.
Lengo la ziara ya Naibu Waziri
Mpina Mkoani Tabora inahusisha ukaguzi wa mazingira, ukaguzi wa
utekelezaji wa agizo la serikali la kupanda miti na ufuatiliaji wa swala
zima la usafi wa mazingira mkoani Tabora ambapo Ripoti ya Mkoa inaema
kwa upande wa swala la usafi wa Mazingira Mkoa umejitahidi.


No comments:
Post a Comment