KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 21, 2016

PLUIJM AITANGAZIA KIAMA KAGERA SUGAR,CHIRWA KUONGOZA MASHAMBULIZI KESHO.

heroa
Na.Alex Mathias.
Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza,Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Der Pluijm ameitangazia vita Kagera Sugar zitakapokutana kesho kwenye uwanja wa Kaitaba mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Akizungumza baada ya kutua mkoani Kagera Pluijm,amesema kuwa anategemea mchezo utakuwa mgumu kwa kila timu kutafuta alama tatu muhimu na ukiangalia wenyeji nao wana alama 18 sawa na sisi ila hilo halitupi shida.
“Kila mechi kwetu tunaichukilia kwa uzito wa aina yake na ukiangalia kikosi changu bado kina uchovu wa mashindano ya kimataifa ndio maana najaribu kufanya mabadiliko mbalimbali ili kuwapa nafasi wachezaji wote wacheze”alisema Pluijm
Timu hizo zinatarjia kukutana kesho huku zikiwa zote zimetoka kupata ushindi Kagera waliwafunga Maafande wa JKT Ruvu kwenye uwanja wa Mabatini wakati Mabingwa watetezi wao waliwafunga wadogo zao Toto mabao 2-0.
Hata hivyo Kocha huyu hakuacha kumsifia mshambuliaji wake raia wa Zambia Obrey Chirwa kwa kuanza kuzoea Ligi na kuanza kujiamini na kufunga magoli mpaka sasa anayo mawili na kuondoa presha za mashabiki ambao walikuwa wanaomuona kama sio mchezaji mzuri.
Kagera Siugar wanawakaribisha mabingwa wao wakiwa chini ya Kocha mpya Mecky Mexime na wakiwa nafasi ya nne kwa alama 18 wakati Yanga wapo nafasi ya tatu kwa alama 18 huku kinara bado Simba anaongoza kwa alama 24.

No comments:

Post a Comment