KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 21, 2016

SAMATTA AING’ARISHA GENK EUROPA LEAGUE,YAICHAPA BILBAO.

Samatta Mbwana Ally forward of Krc Genk looks behind him during the Jupiler Pro League match between Royal Mouscron Peruwelz and KRC Genk in the Le Canonnier Stadium in Mouscron, Belgium. *** MOUSCRON, BELGIUM - 06/02/2016  Photo by Nico Vereecken / Photonews ***
Wakicheza katika uwanja wa Cristal Arena nchini Ubelgiji wenyeji KRC Genk imepata ushindi wa pili michuano ya kombe la Europa baada ya kuwahenyesha Athletic Bilbao jumla ya mabao 2-0.
Kijana wa Kijapan Leon Bailey alikuwa mwiba kwa mabeki wa Bilbao kwani kila muda alikuwa anaichachafya ngome na mnamo katika dakika ya 40 alitoa pasi safi kwa Jakub Brabec na kuiandika Genk bao la uongozi hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa Genk kufanya mabadiliko kwa kumtoa Thomas Buffel na nafasi yake kuchukuliwa na Mtanzania Mbwana Samatta dakika ya 56 kuingia kwa Samatta kulileta uhai tena katika safu ya ushambuliaji.
Samatta alionesha kuwa yeye sio mtu wa mchezo kwa kusababisha bao la pili dakika ya 84 likifungwa na Onyinye Ndidi kwa shuti kali lililoenda moja kwa moja na kuwafanya Bilbao kutoka nje kwa huzuni hadi mwamuzi Stefan Johannesson anamaliza mpira Genk wameibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kwa matokeo hayo Genk wanashikilia usukani mwa msimamo wa kundi F wakiwa na alama 6 wakati Bilbao wana alama 3 na kushika nafasi ya mwisho na Rapid Vienna na Sassuolo zote zikiwa na alama 4 baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1,timu hizi zitarudiana Novemba 3 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment