
BWENI la wanafunzi
wasichana katika shule ya sekondari ya Moreto iliyopo tarafa ya Msoga
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya kuungua kwa moto na
kusababisha mali zote za wanafunzi hao kuteketea kwa moto. (Picha na
Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, ametoa magodoro 50, yenye thamani ya sh.mil
2.225 kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Moreto, waliounguliwa
na bweni lao na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.
Wanafunzi hao
wapatao196, katika shule hiyo iliyopo kata ya Lugoba tarafa ya Msoga,
wilaya ya Bagamoyo, wamenusurika kifo baada ya bweni hilo kuteketea kwa
moto siku ya october 5.
Moto huo umeteketeza mali zote zilizokuwemo ambazo hadi sasa hazijajulikana thamani yake.
Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, Ridhiwani alifika shuleni hapo kutembelea na kutoa pole kwa kutokea janga hilo.
Alisema wakumshukuru ni
mungu kwani pamoja na kutokea kwa hasara ya kuteketea kwa mali lakini
hakuna madhara kwa wanafunzi yaliyotokea.
Ridhiwani aliwapa pole walimu na wanafunzi kijumla na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kwenda kusaidia pale watakapojaaliwa.


No comments:
Post a Comment