Habari na Picha na Robert Hokororo
Mwenge wa Uhuru umewasili na kupokelewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ukitokea Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Uliwasili
majira ya saa 2 asubuhi katika Kijiji ya Bubiki ambapo Mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga, Josephine Matiro alimkabidhi mwenzake wa Wilaya ya
Kishapu, Nyabaganga Taraba kabla ya kuanza mbio zake kukagua na kuzindua
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ukiwa
wilayani humo ulizindua miradi 11 yenye thamani ya sh. bilioni 1.6
ikiwemo ule wa maji kutoka Ziwa Victoria mkoani mwanza unaotarajiwa
kuanza kuwanufaisha wakazi wa Kishapu hivi karibuni.
Mara
baada ya kuwasili wilayani humo mbio za Mwenge wa Uhuru zikiongozwa na
Mkuu wa wilaya hiyo na viongozi mbalimbali ulianza mbio zake kuelekea
katika mradi wa kwanza wa vyumba vipya vya madarasa na matundu ya vyoo.
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali
mara baada ya kuwasili wilayani Kishapu.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Kishapu, Nyabaganga Taraba wakisubiri kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru wilayani humo
katika Kijiji cha Bubiki.
Kikundi cha ngoma cha Makirikiri kikionresha manjonjo
yake katika ufunguzi wa mradi wa stendi kuu ya mabasi na kituo cha polisi eneo
la Mhunze wilayani Kishapu wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru.





No comments:
Post a Comment