KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 22, 2016

SHIRIKA LA IDADI YA WATU DUNIANI (UNFPA) LAZINDUA TAARIFA YA HALI YA IDADI YA WATU DUNIANI

wez1
Mgeni Rasmi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa katika Jukwaa Kuu na viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).  Wengine pamoja nae ni Bw. Barnabas Yisa, Ofisa Mkaazi Mfawidhi UNFPA Tanzania (kushoto) na Mhe. Issa Juma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B (kulia).
wez2
Mhe. Salama Abuu Talib, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
wez3
Wananchi wa kijiji cha Kilombero, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakijiri wakati hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo. 

No comments:

Post a Comment