*Ni katika kukabiliana na ujio wa Serikali Dodoma
MENEJA wa Shirika la Ugavi wa
Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Dodoma, Mhandisi Zakayo Temu amesema ni
vema mkoa huo ukapewa hadhi ya mkoa maalum ili uweze kukabiliana na
changamoto za ujio wa Serikali Dodoma.
Ametoa ombi hilo jana jioni
(Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akitoa taarifa ya utendaji wa TANESCO
Mkoa wa Dodoma mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alifika
kwenye kituo cha kupozea umeme cha Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma,
kukagua mahitaji halisi ya umeme ikilinganishwa na ujio wa watumishi
mkoani humo.
Mhandisi Temu alisema: “Tunaomba
mkoa wetu wa Dodoma ambao ni Makao Makuu uangaliwe kwa jicho la pekee na
kupewa hadhi ya mkoa maalum kama ilivyo kwa Dar es Salaam ambako kuna
mikoa minne ya ki-TANESCO.”


No comments:
Post a Comment