
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva akieleza mkakati wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea
wananchi uelewa sahihi juu majukumu ya Tume na chaguzi zinazofanyika
nchini.
…………………………………………………………………………
Na.Aron Msigwa – NEC. – Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu
Damian Lubuva amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaendelea kutoa
elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi
juu majukumu ya Tume na chaguzi zinazofanyika nchini.Akizungumza jijini Dar es Salaam Jaji Lubuva amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakishindwa kutimiza Haki yao ya Kikatiba ya kupiga Kura kuwachagua viongozi wananowapenda kwa sababu ya kukosa uelewa juu ya Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia Uchaguzi .
Amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 inaipa NEC jukumu la kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa upande wa Tanzania Bara na kubainisha kuwa ili jukumu hilo lifanywe kwa ufanisi wananchi waliotimiza vigezo vya kupiga kura na wale wanaotarajia kupiga kura miaka ijayo lazima wapatiwe elimu sahihi ya Mpiga Kura.
Amefafanua kuwa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, NEC ilianza kutekeleza programu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya Mpiga Kura kuwafikia wananchi moja kwa moja kupitia mikutano mikubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, maonesho ya Sabasaba na Nane Nane , kutoa elimu ya Mpiga kura kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na kuzitembelea baadhi ya shule za Sekondari za mkoa wa Singida na Mara.


No comments:
Post a Comment