Katika
kutekeleza mkakati wa kampuni wa kutunza mazingira na sera ya
wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi za kijamii,wafanyakazi wa
TBL Group wameungana na viongozi wa serikali na wafanyakazi wa taasisi
mbalimbali za kiserikali na za binafsi katika kampeni ya uhamasishaji
upandaji miti inayojulikana kama Mti Wangu.
Kampeni
hii imezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan katika eneo la viwanja vya Gymkhana.
Diwani wa kata ya Kivukoni manispaa ya Ilala Henry Massaba wa pili (kushoto) akimkabdhi mti wa kupanda Meneja Ufanisi wa Uzalishaji Charles Nkondola Charles Nkondola kwa niaba waya wafanyakazi wa TBL Group wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Mti Wangu’ .Kushoto ni Meneja wa Afya na USalama, Renatus Nyanda.
Wafanyakazi wa TBL wakishiriki katika zoezi la kupanda miti katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa TBL wakishiriki katika zoezi la kupanda miti katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.


No comments:
Post a Comment