![]() |
| Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari, kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma. |
![]() |
| Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua jinsi ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kupitia komputa wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Kulia ni Afisa wa Bandari anayeshughulika na ukaguzi, Adam Masoud. |
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma (wapili kushoto), akimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kutembelea bandari hiyo ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na wakwanza kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu. |
![]() |
Kifaa cha kubebea kontena kikiwa
kimebeba kontena tayari kupelekwa kwenye mashine maalumu ya ukaguzi
ambayo hutumia mionzi kukagua mzigo uliopo ndani, ambapo Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza
Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari ya Zanzibar kukagua
mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
Visiwani Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
|






No comments:
Post a Comment