Mkataba
wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA) baina ya nchi wanachama wa Jumuiya
ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Umoja wa
Ulaya (EU), bado halijapatiwa ufumbuzi mpaka hivi sasa.
Baada
ya Tanzania na Uganda kugoma kusaini mkataba huo wa ushirikiano ambao
baadhi ya viongozi wanaufananisha na ukoloni mambo leo, viongozi hao
wamekubaliana kutuma ujumbe mjini Brussels, Ubelgiji yaliko makao makuu
ya EU ili kujadili kwa kina juu ya EPA na kufikia ufumbuzi.
Mwenyekiti
mpya wa jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
atakwenda huko ili kujadili nafasi ya kiuchumi ya EAC na pia kuzungumzia
suala la kutoiadhibu Kenya kutokana na nchi wanachama kutosaini mkataba
huo.
Akizungumza
katika mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za EAC mara baada ya kukabidhiwa
kijiti cha kuiongoza jumuiya hiyo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar
es Salaam jana, Rais Museveni alisema, ataongoza ujumbe huo ndani ya
mwezi kuanzia jana na kwamba EU haipaswi kuiadhibu Kenya kwa nchi
wanachama kutosaini mkataba wa EPA.
“Tutawezaje
kujadili na kusaini mkataba hali ya kuwa mwanachama wetu mmoja
amewekewa vikwazo na EU ? bado tunahitaji ufafanuzi juu ya mambo kadhaa
yaliyomo kwenye mkataba wa EPA,” alisema Museveni.



No comments:
Post a Comment