KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 16, 2017

RAIS WA TFF,JAMAL MALINZI AMSHUKURU AHMED MGOYI


Aa1
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi amempongeza Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ahmed Mgoyi kwa utumushi mara baada ya kutangaza kutowania nafasi yoyote ya uongozi.
Mjumbe Mgoyi anayewakilisha Mikoa ya Kigoma na Tabora aliandika waraka jana Juni 15, 2017 akielezea kutogombea tena katika Uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
“Nimefanya kazi na Wajumbe wangu wote wa Kamati ya Utendaji. Tumefanya kazi kwa uadilifu mkubwa. Wakati Tukielekea kwenye uchaguzi, mwenzetu ametangaza kutogombea tena, lakini kwa namna nilivyofanya naye kazi, kwangu mimi naamini anahitajika mno, lakini uamuzi wake ni mwisho unakuwa ni wa kwao.
“Naamini kwamba bado ni mwanafamilia wa mpira wa miguu na pindi atakapohitajika kwa lolote lile kama vile ushauri na masuala mengine, basi hatutasita kuwafuata kwa sababu lengo ni kujenga na kuendeleza mpira wetu,” amesema Malinzi.
Katika ujumbe wake, Rais Malinzi amesema kwamba hadhani kama Mgoyi hao atasita au kukataa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa shirikisho pindi akihitajika kutoa msaada wao wa mawazo na ushauri.
Rais Malinzi amemtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine aliyojipangia kuyafanya huku akiwa bado mwanafamilia wa mpira wa miguu

No comments:

Post a Comment