Rais wa soka barani Afrka (CAF ) Ahmad Ahmad.
……………………………………………………………………………………….
Shirikisho la Soka barani Afrika
(CAF) limefanya maamuzi ya kuwavua uanachama chama cha soka cha Zanzibar
ikiwa ni miezi minne toka kipewe uanachama na CAF kutoka kwa Rais
aliyepita Issa Hayatou.
Rais wa soka barani Afrka (CAF )
Ahmad Ahmad amesema Zanzibar walipewa uanachama kimakosa na kama sheria
zingepitiwa vizuri wasingepewa uanachama.
“Walipewa uanachama bila kupitia
vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na
sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”
Sababu kubwa ambayo CAF wameivua
uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania
ambao nao ni wanachama wa CAF.
“Jina la nchi linatokana na jina
linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo
inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa
CAF” alisema Ahmad.
Hilo ni pigo kubwa kwa Wazanzibar
kwani wakati huu walikuwa wakipambana kupata uanachama wa FIFA ambao
wameukosa na wa CAF nao pia wamekosa.
Kwa maana hiyo ndoto ya kisiwa
cha Zanzibar kushiriki michuano ya CAF kama mwanachama zimekufa rasmi na
sasa watakuwa wakishiriki michuano hiyo kama Tanzania (Zanzibar na
Tanzania bara).
No comments:
Post a Comment