Mbunge
wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amemuomba Spika wa Bunge, Job
Ndugai alieleze bunge ni lini atawagawia wabunge kompyuta mpakato
(laptop) ili wasiendelee kutumia nyaraka za makaratasi wakati wa
shughuli za bunge.
Amesema
ugawaji wa laptop hizo kwa wabunge ni moja ya ahadi iliyotolewa na
Spika Ndugai kama sehemu ya mkakati wake wa kuliboresha bunge.
Waitara ametoa hoja hiyo bungeni leo Mei 18, alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika akitumia kanuni ya 68 (7).
Akijibu mwongozo huo, Spika Ndugai amesema atalitolea majibu suala hilo baadaye.
No comments:
Post a Comment